Mahakama kuu ya Mombasa imepunguza dhamana ya wana wa marehemu Ibrahim Akasha na wenzao, wanaokabiliwa na ulanguzi wa dawa za kulevya.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Jaji Dora Chepkwonyi amewapunguzia Baktash Akasha, Gulam Hussein, Ibrahim Akasha na Vijaygiri Goswami dhamana kutoka shilingi milioni 30 hadi shilingi milioni tano.

Akitoa uamuzi wake siku ya Jumanne, Jaji Chepkwony pia aliwaondolea washukiwa hao vikwazo vya kutosafiri nje ya nchi, na kuwataka kujulisha afisa wa upelelezi iwapo watahitaji kusafiri.

Aidha, amewataka kupiga ripoti kwa afisa wa uchunguzi mara mbili kwa mwezi, kinyume na hapo awali ambapo walitakiwa kupiga ripoti mara tatu kwa mwezi.

Jaji Chepkwony alisema kuwa alichukua hatua hiyo kwa kuwa washukiwa hao wamekuwa wakihudhuria vikao vya kesi hiyo bila pingamizi.

Haya yanajiri baada ya washukiwa hao kuwasilisha ombi la kupunguziwa dhamana katika Mahakama kuu ya Mombasa.