Mwenyekiti wa wanabiashara katika kaunti ya kisii Elijah Ombongi ameomba serikali ya Kaunti ya Kisii kuwajengea wanabiashara vibanda ili kujikinga na mvua inaponyesha na hata wakati wa jua kali.
Akiongea hiyo jana katika uwanja wa Gusii katika hafla ya uzinduzi wa bendera ya kaunti ya Kisii, Ombongi alikiri kuwa kuna haja wanabiashara kukumbukwa na serikali ya kaunti kwa kujenga vibanda hivyo ili kufanya biashara zao bila kushuhudia changamoto yoyote.
Wakati huo huo, mwenyekiti huyo alimwomba gavana wa kaunti hiyo James Ongwae kuwekea wanabiashara usalama wa kutosha wanapoendelea na ubadilishanaji wao ili kuzuia visa via ukosefu wa usalama dhidi yao, na kutaka kuhakikishiwa usalam na maafisa wa serikali ya kaunti.
Aidha, Ombongi alimuuliza ongwae kufungua mradi wa mikopo kwa serikali yake ili wanabiashara wawe wakikopa na kutumia mikopo hiyo kufanyia biashara zao ili kujiendeleza kimaisha na kuinua uchumi wa kaunti hiyo.
“Gavana wetu ninakuomba kwa unyenyekevu, anzisha mradi wa mikopo kwa serikali yako ili wanabiashara wawe wakikopa mikopo ili kuinua uchumi wa kaunti yetu maana si wanabiashara wote wako na pesa za kutosha kifanyia biashara,” alisema Ombongi.
Uzinduzi wa bendera ya kaunti hiyo uliwaleta baadhi ya viongozi wa eneo la Kisii pamoja na kushukuru serikali ya kaunti kwa hatua hiyo.
Waliohudhuria sherehe hiyo ni gavana James ongwae, naibu wake Joasha Maangi, mbunge wa Kitutu Chache Kusini Richard Momoima, mbunge wa Bonchari Zebedeo Opore na wawakilishi wa kaunti ya Kisii na wengine wengi.