Wanabodaboda wa kituo kilichoko eneo la Mbanda wadi ya Marani eneo bunge la kitutu chache kaskazini kaunti ya Kisii, wako na kila sababu ya kutabasamu baada ya mwakilishi wa wadi hiyo Dennis Ombachi Kuwajengea kibanda cha kujikinga na mvua inaponyesha na hata wakati wa jua kali.

Share news tips with us here at Hivisasa

Benard Ogari, Rodgers Omariba,Peterson Ongori ni miongoni mwa  wanabodaboda ambao walimshukuru mwakilishi huyo wa wadi hiyo ya Marani, wamekuwa wakisumbuka  kwa muda murefu hasa  mvua inaponyesha na wakati huu wa mvua nyingi ambayo inaendelea kunyesha kote nchini.

Aidha, mwakilishi huyo ameahidi kuwafanyia mengi wanabodaboda hao ili kuimarisha sekta ya uchukuzi katika eneo hilo.

“Hatukuwa na mahala pa kujikingia mvua inaponyesha, kwani mahala hapa hakuna nyumba na tumekuwa tukinyeshewa kwa muda mrefu lakini kwa sasa tunafurahia mwakilishi wetu ,kwa kutujengea kibanda hiki na tunampongeza na tunamwomba mwakilishi  aendelee kufanya maendeleo ya aina hiyo,” alihoji Ogari mwanabodaboda.

Wanabodaboda wa wadi hiyo wamekuwa wakisumbuka kwa muda mrefu, kutokana na ukosefu wa vibada huku wengi wao wakisema kila kituo katika wadi hiyo kinastahili kuwa na kibanda cha wanabodaboda ili kufurahia matunda ya ugatuzi ambayo wengi wanasubiri kushuhudia kabla ya miaka mitano kukamilika .

“Ni vizuri serikali za ugatuzi zilianzishwa nchini, maana hatungekumbukwa kama sisi wanabodaboda lakini ugatuzi umetuwezesha tumekumbukwa, tunafurahia kwa kiwango cha juu zaidi,”alisema Ongori mwanabodaboda.