Waendesha wa bodaboda katika kaunti ya Nyamira wameshauriwa kujisajili kwa bima ili kupata usaidizi wakati wanapohusika katika visa vya ajali barabarani.
Wito huo umetolewa baada ya uchunguzi kuonyesha kuwa idadi kubwa ya waendeshaji bodaboda katika kaunti ya Nyamira hawajajisajili kwa bima hiyo ili kupata usaidizi wakati pikipiki zao zinapohusika kwa ajali, kuibwa miongoni mwa visa vingine.
Akizungumza mnamo siku ya Alhamisi mjini Nyamira, mshauri mkuu wa bima katika kaunti ya Nyamira Richard Mosota aliwaeleza waendeshaji hao umuhimu wa kuwa mmoja wa waliosajiliwa kwa bima, huku akiwashauri kufanya hivyo ili kutopata hasara kubwa katika siku zijazo.
“Naomba kila mwendeshaji pikipiki kusajiliwa kwa bima ili unapopata ajali unaweza fadhiliwa ikiwa pikipiki yako imearibika kupita kiasi, unaweza kulipwa ikiwa hauko barabarani kutokana na ajali, pikipikipi ikiibiwa miongoni mwa mengine,” alisema Richard Mosoti, mshauri wa bima.