Wanachama wa Muungano wa Jubilee katika Kaunti ya Mombasa wameikosoa serikali ya kaunti kwa madai ya kushindwa kuwajibikia majuku yake kikamilifu, sambamba na kuwahudumia wakaazi jinsi katiba inavyoangazia.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho tawi la Mombasa Sharrif Shekue amesema kuwa Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho anafaa kuwatekelezea wakaazi maaendeleo mashinani kabla ya kuwania urais.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumatano, Shekue alisema kuwa kuna maswala muhimu ya kutekelezwa kwa sasa ikiwemo miundo msingi, ukarabati wa mitaro ya kupitisha maji taka, elimu na maswala mengine muhimu, wala sio kujishughulisha na siasa za mapema.

"Tunaitaka serikali ya Kaunti ya Mombasa Kuhakikisha kuwa inatekeleza maswala muhimu ya kaunti wala sio kudanganya wakaazi na mambo ya kisiasa,” alisema Shekue.

Kiongozi wa walemavu katika muungano huo wa Jubilee tawi la Mombasa Naftan Swaka ameitaka serikali ya kaunti hiyo kuhakikisha kuwa inatenga fedha zaidi katika bajeti ya mwaka ili kuwasiadia walemavu.

"Serikali ya Kaunti ya Mombasa imewasahau kabisa walemavu na kuwaacha wakihangaika katikati ya mji na sisi ndio tuliipigia kura katiba na kuwapitisha viongozi wa sasa,” alisema Swaka.