Wanachama wa shamba la Ng’ati huko Naivasha wanamtaka rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati mzozo unaokumba usimamizi wa shamba hilo ili waweze kupata suluhu.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wanachama hao walisema wamekuwawakipitia shida nyingi kwa karne kadhaa huku serikali za hapo awali zikiwatelekeza.

Aidha walihoji ni kwa nini rais Kenyatta amekuwa akiingilia kati mizozo ya ardhi ambapo jamii zingine zinahusika lakini amekaa kimya wao wakiumia licha ya kuwa wamekuwa wakimuunga mkono kisiasa.

“Wakati ambapo kulikuwa na mzozo huko Narasha, rais Kenyatta pamoja na naibu wake walifika huko na kutatua mara moja. Lakini sisi wakikuyu hataki kuingilia kati, ni kwa nini,” Mary Nyambura alisema.

Wanachama hao walisema rais amekuwa akisuluhisha mizozo mingine nan i jambo la kusikitisha kuwa amekataa kutatua mzozo wa wafuasi wake.

“Juzi alikuwa huko Mombasa na akatatua mzozo wa Waitiki, watu wa Mau walitatuliwa mizozo yao, mbona Uhuru amekataa kuingilia hapa Ng’ati?” mkaazi mwingine alisema.