Chama cha RBM Credit kikishirikiana na shirika la Vision Fund kimewanunulia wanachama wao kadi za matibabu za NHIF bila malipo.
Akizungumza na wanahabari siku ya Jumamosi katika mji wa Kisii, mwenyekiti wa chama cha RBM Credit Lumumba Nyaberi alisema wanachama wale wamechukuwa mikopo kutoka chama hicho watanunuliwa kadi za NHF bila Malipo, huku wanachama ambao wamejisajili wakiwa 12,000 na tayari wanachama 6,000 wamenunuliwa kadi hizo.
Chama hicho cha RBM Credit kiliwanunulia wanachama hao kadi hizo kupitia kampuni ya Jubilee, huku wakiambiwa kuwa mwanachama akiwa mgonjwa na apelekwe hospitalini kadi hizo zitagharamu hadi 200,000, huku mwenyekiti huyo akisema wale ambao wamebaki watanunuliwa hivi karibuni.
“Kadi hizi tumewanunulia mmoja akiwa mgonjwa itagharamia pesa za hospitali hadi shillingi 200,000 na mgonjwa akipitisha hapo basi zingine atajitolea mwenyewe,” alihoji Nyaberi.
Chama hicho cha RBM kimehudumia wakaazi wa kaunti ya Kisii kwa miaka mitano, huku wakitoa shillingi 1,000,000 kwa chama kimoja ambacho kina wanachama 40.
Aidha, Mwenyekiti huyo alisema hiyo ndiyo njia mojawapo ya kuinua uchumi katika kaunti ya Kisii, ili watu kujiusisha katika sekta ya biashara.
“Kama watu wengine wanahitaji kujiandikisha katika chama hiki cha RBM Credit, mlango uko wazi, tunawaalika waje wajiandikishe wapate mikopo wafanyie biashara, lengo letu ni kuinua kaunti hii kiuchumi,” aliongezea Nyaberi.