Viongozi wa wa wadi mbalimbali wametakiwa kuzingatia watoto maskini na walio na matokeo ya kufana wakati wa kupeana hela za kuwasaidia masomoni ili kufanikisha zoezi hilo.
Haya ni matamshi yake gavana wa jimbo la Nakuru Kinuthia Mbugua katika hafla ya kuwahisani wanafunzi kumi na wawili kutoka familia maskini katika jimbo la nakuru ili kuwawezesha kujinga na shule za upili.
Katika taarifa yake, Gavana huyo amesema kuwa serikali yake itazidi kuwekeza katika sekta ya Elimu sawia na Afya kama njia moja ya kukabiliana na kero la umaskini katika jimbo.
Wanafunzi hao aidha waliojumuisha wasichana watatu na wavulana tisa ni miongoni wa maelfu ambao walipata nafasi za kujiunga na shule za kitaifa na kukosa uwezo kwa kuzingatia hali yao ya maisha.
Akiongea katika hafla hiyo, waziri wa elimu katika jimbo la nakuru Catherine Kitetu amewapa changamoto washikadau sawia na wawekezaji katika jimbo kutoa msaada yao kwa wanafunzi kama hao, akitaja kuwa wengi wa waliofuzu katika mtihani huo ni wale kutokaa familia maskini.
Kitetu aidha amewahimiza wazazi kuhakikisha kuwa wale wanafunzi ambao hawakupata nafasi katika shule za upili kufuatia matokeo yao duni wamejiandikisha ili kupata nafasi katika vyuo vya anuai.
Vilevile, naibu wa gavana Joseph Rutto amewapa changamoto viongozi wengine katika jimbo na hata serikali kuu kujitolea na kuwasaidia baadhi ya wanafunzi wanaohitaji msaada na wala sio kungojea kukosoa huduma zinazotolewa na wengine .
Hata hivyo, chini ya mpango ‘Kinuthia Mbugua Foundation’, wanafunzi hao walipokea shilingi elfu mia nane za kuwawezesha masomo yao ya mwaka huu.