Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Kisii Mary Otara amewafadhili wanafunzi 819 ili kujiendeleza kimasomo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wanafunzi hao walipata ufadhili huo wa basari kupitia hazina ya Wawakilishi wa wanawake kwa jina 'National Government Affirmative Action Fund' ili kuendeleza masomo.

Akizungumza siku ya Jumatano mjini Kisii wakati alipotoa ufadhili huo Otara alisema wanafunzi 138 wa vyuo vikuu ndio walifadhiliwa huku wanafunzi 681 wa shule ya upili pia wakipata ufadhili huo.

“Kila eneo bunge lilitengewa millioni 450,000 ili kufadhili wanafunzi wa maeneo bunge hayo ili kujiendeleza kimasomo,” alisema Otara.

“Masomo ni ya muhimu na tunahitaji kila eneo liwe na wasomi ambao watakuwa viongozi wa kesho katika taifa letu,” aliongeza Otara.

Wakati huo huo, Otara aliwaomba wanafunzi wote katika kaunti hiyo kuweka bidii na motisha masomoni ili waje kujisaidia katika siku za usoni.

“Masomo ni ya muhimu zaidi na sharti kila aliye shuleni kuweka bidii katika masomo,” alisistiza Otara.