Wanafunzi wakifanya mtihani hapo awali. [Picha/ capitalfm.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Wanafunzi waliohamishwa kutoka eneo la Boni hadi shule ya msingi ya Arid Zone kutokana na uhaba wa walimu wanatarajiwa kufanya mtihani wa kitaifa wa KCPE hapo kesho.Wanafunzi hao wamesema kuwa wako tayari kufanya mitihani hiyo licha ya matatizo mbali mbali waliyokumbana nayo.Mwalimu mkuu wa shule ya Arid Zone Abubakar Ruhuma amewatia moyo wanafunzi hao na kuwaambia kuwa watafaulu mtihani huo, hatua aliyosema itawawezesha kusaidia familia zao katika ziku za usoni.Ruhuma alisema kuwa ana imani kuwa wanafunzi hao watafanya vyema kwenye mtihani huo wa kitaifa.“Nina imani kuwa wanafunzi hawa watafanya vyema katika mtihani wao wa KCPE,” alisema Ruhuma.Shule zote katika Wadi ya Basuba, eneo la Boni zilifungwa kutokana na ukosefu wa walimu kufuatia mashumbulizi ya kundi la al-Shabaab yalishohudiwa katika eneo hilo.Wanafunzi wa kuanzia darasa la nne kutoka eneo hilo walipelekwa katika shule ya Arid Zone.Shule hiyo ina wanafunzi 42 wanaotarajiwa kuanza mtihani wao wa kitaifa hapo kesho (Jumanne).Takriban wanafunzi 2,384 wa darasa la nane Kaunti ya Lamu wanajitayarisha kuanza mtihani wao wa KCPE.Oliver Muthomi, ambaye ni msimamizi wa mtihani katika Shule ya msingi ya Arid Zone amedokeza kuwa wako tayari kusimamia mtihani huo.Muthomi alisema kuwa watahakikisha hakuna udanganyifu wa aina yoyote ambao unashuhudiwa.