Maafisa wa polisi mjini Molo wanaendelea kuchunguza kisa ambapo wasichana wanne wa shule ya upili mjini humo wamekodisha yyumba wanayoitumia kama danguro badala ya kuhudhuria masomo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Sakata hii imeibuka baada ya wananchi kuwapasha habari maafisa wa polisi pamoja na chifu wa eneo hilo Hassan Waweru ambao walivamia Nyumba hiyo na kuwafumania wasichana hao pamoja na wanaume wawili ambao walifanikiwa kutoroka.

Wasichana hao wamesema wao hutoka nyumbani alfariji na badala ya kwenda shule, wao huelekea katika nyumba hiyo ya burudani ambapo tabia sisizoelezeka hutekelezwa.

Zaidi ya chupa 20 za pombe aina tofauti zilipatikana huku wenyeji wakibaki vinywa wazi kuona utovu wa maadili ulivyoadhiri kizazi cha sasa.

Chifu Waweru amesema huenda wanafunzi hao wamekuwa katika biashara hiyo kwa muda mrefu akisema uchunguzi utaendelezwa ili kubaini wahusika wote ambao wanachangia.

Walimu katika shule hiyo wamesema wanafunzi hao wanne hawahudhurii masomo huku wakidai ukosefu wa karo miongoni mwa vijisababu vingine.

Aidha wanafunzi hao wamedinda kutambua wanaume wawili ambao walifanikiwa kutoroka na ambao kwa sasa wanasakwa na maafisa wa polisi.

Wanafunzi hao ni wa kati ya miaka 15 na 17 ambao wanasoma kidato cha pili na cha tatu.