Mwakilishi wa wadi ya Nyamira mjini, mheshimiwa Robert Ongwano, amewaonya wanafunzi watahiniwa wa darasa la nane na kidato cha nne dhidi yakujihusisha na visa vya udanganyifu katika mitihani ya kitaifa ya mwaka huu.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akihutubia makundi mbalimbali ya walimu kwenye chumba cha mikutano huko Nyamira siku ya Ijumaa, Ongwano aliwasihi wanafunzi hao kujiamini kwa matokeo bora.

"Nawaonya watahiniwa wote dhidi yakujihusisha na visa vya udanganyifu wa mitihani ya kitaifa ya mwaka huu na ninawasihii wajiamini kwa matokeo mazuri,” alisema Ongwano.

Ongwano aidha aliongeza kwa kusema kuwa kaunti ya Nyamira imekuwa miongoni mwa kaunti zinazo jihusisha na visa vya udanganyifu katika mitihani katika siku za hapo awali, swala ambalo alisema halifai kujitokeza tena mwaka huu, kwa kuwa huenda likaathiri matokeo ya mitihani.

Aidha, amewasihi walimu kuheshimu uamuzi wa mahakama na kurejelea majukumu yao ya kawaida kwa kuwa mgomo wao umewaathiri pakubwa wanafunzi wa shule za umma.

Ongwano aliwasihi walimu kusitisha mgomo wao ili kuvipa vyama vyao pamoja na serikali nafasi yakujadiliana kuafikia suluhu la mgomo huo.

"Nawaomba walimu wote kukubali nakuheshimu uamuzi wa mahakama na kurejea darasani ili kuvipa nafasi vyama vyao pamoja na serikali kushauriana kuafikia suluhu la haraka,” alisema Ongwano.