Chuo kikuu cha Pwani kimekumbwa na hali ya sintofahamu baada ya wanafunzi wa chuo hicho kujaribu kukichoma mwendo wa saa nane usiku.

Share news tips with us here at Hivisasa

Usimamizi wa chuo hicho umesema kwamba wanafunzi watano wamenaswa wakiwa na mafuta aina ya petroli wakiwa tayari kuteketeza baadhi ya majengo.

Naibu chansela wa chuo hicho Professa Rajab Mohamed amesema amewajulisha maafisa wa polisi eneo hilo ambao walifika tayari kuwakamata wanafunzi hao lakini wakawa wametoroka.

Aidha, Rajab amesema kuwa wanafunzi hao watalazimika kuondolewa katika chuo hicho pindi tu uchunguzi utakapokamilika.

Hata hivyo, ameongeza kuwa huenda hatua ya wanafunzi hao ikawa inasababishwa na hatua ya usimamizi wa chuo hicho ya kuwafukuza wanafunzi waliokuwa wakiongoza migomo.