Katika njia mojawapo ya kuona vijana wanapata kazi katika kaunti, gavana wa Kisii James Ongwae, ameahidi kuwapa vijana wa Chuo Kikuu cha Kisii kazi kusaidia katika kuweka na kuratibu rekodi za sajili ya idara ya Ardhi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Gavana huyo alikuwa akizungumza siku ya Ijumaa katika ofisi yake, baada yake kushiriki kufunga operesheni ya Idara ya Usajili ya Ardhi na waziri wa kaunti. hiyo ya Kisii Moses Onderi.

Shughuli hiyo ya kuratibu na kupanga data za idara ya ardhi itaanza wiki ijayo, huku gavana Ongwae akisema kuwa tayari anapanga kuongea na usimamizi wa chuo hicho cha Kisii ili kushirikisha wanafunzi ambao wanafanya taaluma ya Technolojia ya Mawasiliano kuorodhesha rekodi zote kwenye ofisi hiyo katika mtandao ili kuwa rahisi kufuatilizia rekodi hizo.

“Nitaongea na chuo chetu cha Kisii ili kuwashirikisha wanafunzi. wa kitengo cha mawasiliano cha chuo hicho kufanikisha shughuli hiyo,” aliongezea Ongwae.

Ongwae alisema pia kuwa hii itaepusha ufisadi na kurahisha mafisaa wa idara hiyo kufikia rekodi za watu kuhusiana na ardhi na zile ardhi ya umma kidijitali.