Huku shule zikifunguliwa leo, wanafunzi wa darasa la kwanza wanatarajia kupokea vipakatalishi katika kaunti mbalimbali humu nchini.
Vifaa hivi vitapeanwa katika shule 150 ambazo zimeteuliwa katika kaunti zote ikiwa Mombasa na Kwale ndizo zitakua za kuanzia kufaidika na mradi huo. Kaunti zitakazozofuata baadaye ni, Garisa, Kisumu, Homabay, Kisii, Uasin Gishu, Kakamega, Bungoma na Kajiado.
Zoezi la kutoa vipakatalishi hivyo linatarajiwa kukamilika tarehe 13, mwezi huu. Tayari shule nne zilipokea mashine hizo mwezi marchi katika awamu ya majaribio.
Kutoa vipakatalishi kwa wananfunzi wa darasa la kwanza ilikua ni moja kati ya ahadi za mrengo wa Jubilee ulipochukua hatamu ya uongozi 2013. Hii itafanyika huku uchaguzi mkuu ujao ukikaribia mwaka wa 2017.