Naibu wa chuo kikuu cha Egerton Profesa James Tuitoek, Ijumaa, aliwaongoza wanafunzi na wahadhiri wa chuo hicho kuadhimisha siku kuu ya mazingira duniani.

Share news tips with us here at Hivisasa

 Prof. Tuitoek aliwahimiza wanafunzi na wahadhiri waliohudhuria maadhimisho hayo kupanda miti ili kutunza mazingira.

 Akiongea katika hafla iliyoandaliwa katika shule ya msingi ya Kilimo iliyomo chuoni humo Profesa Tuitoek aliwapongeza waandalizi wa hafla hiyo ambayo ililingana na wiki ya upanzi wa miti shuleni humo.

 “Chuo cha Egerton Kimejitolea kushirikiana na washikadau wengine ili kuboresha mazingira kwa niaba ya vizazi vijavyo,” alisema Tuitoek.

 Aliongeza kuwa ipo haja ya kutunza miti iliyopandwa ili kuhakikisha kwamba hainyauki.

Aidha aliwapa changamoto kuzidi kupanda miti zaidi huku akiongeza kuwa yeye ataendelea.

“Ni jukumu la kila mtu kuyalinda mzingira kwa kutotupa taka ovyo kwani hio pia ni njia ya kutunza mazingira,” akaongeza Tuitoek.

Chuo cha Egerton kimekua kikiandaa juma la utunzaji wa mazingira na upanzi wa miti kwa miaka kumi na miwili iliyopita kwa azimio la kuboresha mazingira chuoni humo na katika maeneo mengine.