Wanafunzi wanane katika shule ya upili ya wasichana ya Nyamagwa kaunti ya Kisii wamefikishwa katika mahakama ya Ogembo na kushtakiwa kwa kudaiwa kuhusika na kuchoma bweni la shule hiyo mnamo machi 21 na 22, 2016.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wanafunzi hao walifikishwa mahakamani siku ya Alhamisi huku wakikanusha madai hayo mbele ya jaji wa mahakama hiyo Caroline Ateya.

Wakili wa wanafunzi hao Kepha Mogire alisema mwalimu wa shule hiyo aliwachapa na kuwalazimisha kuitikia kuwa ni wao walichoma bweni la shule hiyo walipotiwa mbaroni tarehe 22 mwezi huu, ambapo walizuiliwa katika mahakama ya watoto ya Manga na kufikishwa kwa mahakama ya Ogembo hiyo Alhamisi.

Aidha, wanafunzi hao waliachiliwa kwa dhamana ya laki moja kila mmoja huku kesi hiyo kutangazwa kuzikizwa tena Aprili 15, 2016.