Mwenyekiti wa chama cha kupambana na dawa za kulevya Kaunti ya Kisii Enes Nyandwaro amesema idadi ya wanafunzi wanaojihusisha na dawa za kulevya imeongezeka.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza siku ya Jumatano katika ukumbi wa  chuo hicho cha Kisii Nyandwaro amesema kuwa vijana wengi wamendelea kujihusisha na madawa ya kulevya.

“Kuna wanafunzi wengi ambao wamepatikana wakilevya. Kama wanachama tumepeleka baadhi ya wao katika vituo vya ukarabati almaarufu kama rehabilitation centres,” alisema Nyandwaro.

Aliendelea kusema kuwa shule kuu ya Kisii ni moja wapo wa shule ambazo ziko na wanafunzi wengi ambao wanajiingiza kwa ulevi.

“Shule hii ni moja ya zile ambazo ziko na watu wengi ambao wamejiingiza kwa madawa ya kulevya,” alisema Nyandwaro.

Wakati uo huo, Nyandwaro alisema kuwa kuna baadhi ya wafanyikazi wa chuo hicho ambao wamejiingiza kwa ulevi.

“Hatuwezi kuwasimamisha kazi wafanyikazi hawa ambao wanafanya kazi hapa na wamejiingiza kwa ulevi lakini tunajaribu kuwasaidia,” aliongeza Nyandwaro.