Huku mgomo wa walimu ukiendelea kote nchini kwa wiki ya pili sasa, idadi kubwa ya wanafunzi inaendelea kushuhudiwa  katika maktaba ya kitaifa iliyoko katika jimbo la Nakuru.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Imebainika kuwa wengi wa wanafunzi hao ni wale wanaotarajia kuukalia mtihani wa kidato cha nne, sawia na darasa la nane mwaka huu.

Mahojiano ya moja kwa moja na watahiniwa watarajiwa hao yamedokeza  kuwa wana hamu kuu ya kurudi kuendelea na masomo yao, licha ya walimu wao kugoma.

Afisaa wa teknologia ya mawasiliano Kaunti ya Nakuru, Josek Olala katika maktaba ya kitaifa tawi amedokeza kuwa idadi ya wanafunzi imeongezeka kwa kiwango kikubwa.

“Tumepata idadi ya wanafunzi wanaozuru maktaba yetu na ambayo bado inazidi kuongezeka kila kuchao, na jambo hili limechangiwa na kuwepo kwa mgomo wa walimu kote nchini,” alisema Olala.

 Aidha, Olala amewataka wazazi kuwaruhusu watoto wao kwenda kwenye maktaba zilizoko karibu. hasaa wakati huu ambapo mgomo wa waalimu bado unaendelea. akisema kuwa inaweza kuchangia katika  kuimarisha kiwango chao cha masomo

 Hatua hii inajiri huku chama cha walimu Knut na Kuppet vikiwa bado vimeshikilia msimamo wao wa kutorudi shuleni , hadi pale serikali itatimiza matakwa yao.