Wanafunzi wa shule ya upili ya Muleleshwa kaunti ya Nakuru waligoma kutokana na mazingira machafu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wanafunzi hao walimlaumu mwalimu mkuu wa shule hio kutokana na masaibu yao. Walidai anafuga mifugo wa kibinafsi katika shule hio wanaochafua mazingira ya shule na kuyafanya yasiwe safi ya kusomewa.

"Ata huwezi keti chini kwa kuwa kinyesi cha ngombe kitakupata makalioni"alisema kamau, mwanafunzi wa kidato cha pili.

"Hawa kuku wanaingia darasani na matope na kuchafua viti vyetu na kufanya kunuke," mwanafunzi mwingine alisema.

Juhudi za mwandishi huyu kuwasiliana na mwalimu mkuu wa shule hio ya Muleleshwa hazikufua dafu baada ya kukataa kuzungumzia swala hilo.