Wanafunzi kutoka shule nyingi katika kaunti ya Nyamira walifika shuleni na kutumwa karo ya shule wakati shule zlifunguliwa kwa muhula wa pilli wiki hii. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hii ni baada ya walimu wakuu katika shule kusema kuwa wazazi wengi hawachukui jukumu lao kama wazazi na kuwalipia wanao karo ya shule na kufanya mipango ya shule kutatizika. 

"Wazazi wengi katika eneo letu la Nyamusi wamelichukulia jambo hili kuwa msaa kwa kutowalipia watoto wao karo kwa muda ufaao, hii hasa ndio inafanya kupoteza muda mwingi unaofaa kutumiwa darasani kwa kutumwa nyumbani kila ujao," alisema mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Matongo. 

Aidha mwalimu huyo amewataka wazazi kuwajibika na kujua kuwa kulipa karo ni jukumu lao hili watoto katika eneo hilo wapate kuelimishwa vyema.