Share news tips with us here at Hivisasa

Wakfu wa Shariff Nassir unaofadhiliwa na Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir, ukiungana na serikali ya Kaunti ya Mombasa, umewatuza wanafunzi, walimu na shule zilizofanya vyema katika mitihani ya kitaifa ya mwaka uliopita.

Akizungumza siku ya Jumamosi katika hafla hiyo, Nassir alisema kuwa wakfu huo unalenga kuboresha elimu katika Kaunti ya Mombasa kwa kuwatambua wanafunzi wanaofanya vyema katika mitihani ya darasa la nane na kidato cha nne.

Gavana wa Mombasa Hassan Joho aliwahakikishia wakaazi wa Mombasa kuwepo kwa umoja baina ya Shirika hilo la Shariff Nassir na serikali ya kaunti.

Aidha, aliongezea kuwa watakuwa wakiwapa watahiniwa chakula wakati wa mitihani hiyo ya kitaifa.