Wanafunzi katika wadi ya Kabatini Nakuru wameanza kunufaika kutokana na ufadhili wa elimu.
Mwakilishi wa wadi hiyo Peter Mwangi alisema kuwa wanafunzi wote kutoka familia zisizojiweza watanufaika.
Kwa mujibu wake, fedha hizo zitapeanwa kwa wanafunzi katika shule tofauti kama vile St Joseph Kirima, St Francis na King David.
Wakati huo huo, MCA Mwangi ametoa wito kwa wazazi kujitokeza ili kujua namna fedha hizo zinavyopeanwa.
"Ningependa kuwarai wazazi wajitokeze kwani swala hilo litakuwa wazi mno" MCA Mwangi alisema.
Vilevile ametoa wito kwa wanafunzi wanaopata fedha hizo kutumia vyema fursa hio kujiendeleza kimasomo.