Wanafunzi katika viungani mwa Kibera wameshauriwa kutohusika kwa ulevi msimu huu wa likizo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mara nyingi humu Kibera wanafunzi wamegundulika kujiushisha na ulevi, jambo ambalo linaathiri masomo yao kwa sababu wanafunzi wakati wa likizo huanza kubugia pombe na hii uharibu maisha yao.

Akizungumza leo asubuhi katika eneo la Olympic, Alice Ayuma ambaye ni mwalimu aliwaomba wanafunzi kupumzika na wazazi wao nyumbani wakati huu wa likizo ndefu kwa sababu hakuna masomo ya ziada na wajiepuze na makundi ambayo yatachangia wao kunywa pombe.

“Pombe inaathiri akili ya mwanafunzi yeyote na pia kudhoofisha afya ya mnywaji. Naomba kila mwanafunzi ahusike na mihadharati na ulevi. Watenga muda na kusoma somo ambalo hawakufanya vyema wanaposubiri shule kufunguliwa,” alisema Alice.

Aliongeza kuwa pombe ndio uharibu maisha ya wengi haswa wanafunzi kuacha shule na kuvunja ndoa nyingi, na kuwaomba wazazi wote kuhakikisha wanafunzi wako na mienendo mzuri wakati huu wa likizo.