Wanafunzi wote katika kaunti za Kisii na Nyamira wameshauriwa kutohusika kwa ulevi katika msimu huu wa likizo.
Ushauri huo umetolewa baada ya kugundulika kuwa wakati wa likizo, baadhi ya wanafunzi huanza kubugia pombe na kuanza kuharibu maisha yao.
Akizungumza siku ya Jumatatu mjini Nyamira, seneta wa kaunti hiyo Kennedy Okong’o aliwaomba wanafunzi kupumzika na wenzao nyumbani wakati huu wa likizo kando na kunywa pombe
“Pombe inaathiri na kudhoofisha afya unapoikunywa, naomba kila mwanafunzi kutohusika kwa ulevi someni na kupumzika nyumbani mnaposubiri shule kufunguliwa,” alisema Okong’o.
Aidha, seneta huyo alisema pombe ndio uharibu maisha ya wengi, na kuwaomba washkadau wote wa sekta ya elimu kushirikiana na kuinua viwango vya masomo juu katika kaunti ya Nyamira
“Elimu ndio msingi kwa kila maisha ya mtoto, sharti sote tushirikiane tuinue viwango vya elimu juu katika kaunti yetu ya Nyamira,” aliongeza Okong’o.