Wanafunzi wa chuo kikuu cha Kisii wameshauriwa kuzingatia maadili wanapotumia mtandao wa shule, maarufu kama wifi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya uchunguzi kuonyesha kuwa wengi wao wamekuwa wakitumia mtandao huo kujiburudisha badala ya kutumia katika kufanya utafiti kwenye masomo yao.

Mwenyekiti wa idara ya mawasiliano na technologia chuoni humo Prof Kurgat amegadhabishwa na tabia hii.

“Ni jambo la kusikitisha na kutamausha kuona wanafunzi wakitumia rasilimali za shule kufanya vitu ambavyo haviambatani na elimu. Nimeghabishwa mno,” alieleza.

Si ajabu kuwakuta wanafunzi wakiwa kwenye mitandao ya kijamii kama vile facebook, twitter wakiwasiliana wakati wanapofaa wakuwe wakisoma kwa bidii.

Ni wiki jana ambapo mmoja wa wanafunzi alipatwa akitizama filamu za ngono kwenye wavuti wa youtube, lakini hakuona haya yoyote.

“Huu mtando ni wa bure, kwa hiyo kile ninachofanya ni kulingana na uamuzi wangu,” alisema

Kulingana na Prof Kurgat, kuna mipango madhubuti ambayo ikikamilik,a idara ya mawasiliano na teknolojia itakuwa na uwezo wa kuwazuia wanafunzi kutumia mitandao flani kwa mfano ile mitandao ambayo haiambatani na elimu.

“Wanafunzi yafaa wakadirie maisha yao ya usoni kwa kutia bidii masomoni na wajitenge na mitandao ambayo haina manufaa kwao kielimu,” alisistiza kwenye mahojiano.