Shughuli ya kuwatambua wanafunzi watakaopokezwa busari katika wadi ya Gesima, eneo bunge la Kitutu Masaba, kaunti ya Nyamira, wametambuliwa.
Akiongea siku ya Alhamisi katika ofisi ya mwakilishi wa wadi ya Gesima, eneo bunge la Kitutu Masaba, naibu mwenyekiti wa kamati iliyoteuliwa kuwatambua wanafunzi hao, Peter Minyira, alisema kuwa wanafunzi hao wote wametambuliwa na sasa watafikisha ripoti kwa mwakilishi wao ili kubaini kiasi cha pesa kila mmoja atapokezwa.
“Kamati hii imetambua wanafunzi wote katika wadi hii ya Gesima watakaopezwa pesa hizo hili kujiendeleza na masomo yao,” alisema Minyira.
Kwa upande wake mwakilishi wa wadi ya Gesima, Kennedy Nyameino, alisema kuwa wanafunzi watapokezwa pesa hizo na orodha ambayo imepatikana ndio itawasaidia kubaini kiwango cha kutoa pesa kwa kila mwanafunzi.
Aliongezea kuwa ikiwa pesa hizo hazitatosha watarudi bungeni ili kujadiliana na kiwango hicho kuongezwa.
Kamati hiyo ambayo iliteuliwa na mwakilishi huyo wa wadi ya Gesima, ilizuru kila shule ya Upili katika wadi hiyo ili kutambua wanafunzi hao.
Naibu wa mwenyekiti allisema kuwa walitambua wanafunzi hao kutokana na mahali wanapotoka haswa katika familiia maskini ili kuwasaidia kuendelea kusoma na kuwalipia karo ya shule.
Kwingineko wakaazi wa wadi hiyo wamemuomba mwakilishi wao kuhakikisha kuwa pesa hizo zimegawa kwa njia ya uwazi na haki ili kila mwanafunzi anayestahili kupata pesa hizo apokezwe.
Wakaazi hao wamesema kuwa pesa hizo zinastahili kutolewa muhula wa kwanza ili kuwasaidia wazazi kulipa karo haswa kwa wale wanafunzi wa kidato cha kwanza.
“Pesa hizi za busari tunaomba kutolewa wakati wa muhula wa kwanza ndio zitusaidie pakubwa,” alisema Daniel Mokaya, mkaazi.