Mbunge wa eneo la Mugirango Kusini kaunti ya Kisii Manson Nyamweya amesema wanafunzi wa shule za msingi, upili na vyuo vikuu katika eneo lake wataanza kupata pesa za basari kuanzia juma lijalo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Nyamwenya alisema shughuli ya kupeana pesa hizo imekuwa ikichelewa kwa kile alichokisema ni kutopata pesa mapema katika Hazina ya Ustawi wa maeneo Bunge (CDF) huku akisema sasa pesa hizo zimeingia na wanafunzi wataanza kupokea kuanzia juma lijalo ili kuendeleza elimu zaidi.

Akizungumza siku ya Jumatano usiku kwenye mahojiano katika kituo cha radio Citizen,  Nyamweya alisema yeye kama mbunge yuko katika mstari wa mbele kuhakikisha elimu imesonga mbele katika eneo bunge lake.

“Nataka kuwahakikishia wakaazi wa eneo bunge langu kuwa pesa mbazo nimekuwa nikisubiri zimeingia na wanafunzi watapata pesa zao za basari baada ya kutuma maombi na nitahakikisha viwango vya elimu vimeinuka katika eneo bunge langu la Mugirango Kusini,” alisema Nyamweya.

Aidha Nyamweya aliwaomba washikadau wa elimu kushirikiana kuinua viwango vya elimu katika kaunti ya Kisii ili wanafunzi wapite katika mitihani ya kitaifa.