Wavulana wawili na msichana mmoja wenye umri wa chini ya miaka 18, wametiwa mbaroni katika eneo la Likoni, kwa madai ya kuhusika katika visa vya ugaidi na ujambazi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akithibitisha kisa hicho siku ya Jumapili, mkuu wa polisi eneo la Likoni Willy Simba, alisema vijana hao walinaswa katika mtaa wa Mbuzi huko Likoni.

“Kweli tumewakamata vijana hao ambao walikuwa wanawasumbua sana wakaazi hasa wakati wa usiku katika eneo la mtaa wa Mbuzi,” alisema Simba.

Aidha, Simba amewataka wakaazi wanaosemekana kuvamiwa na kuibiwa mali yao na vijana hao kujitokeza na kuandikisha ripoti katika kituo cha polisi.

“Tutawafikisha washukiwa hawa mahakamani na kuwafungulia mashtaka,” alisema Simba.

Vijana hao, wenye umri wa miaka 15 na 16, wanaripotiwa kuwa wanafunzi wa shule moja ya upili eneo la Likoni.