Wanafunzi watatu wa Shule ya upili ya Shimo la Tewa wamekamtwa na maafisa ya polisi baada ya kupatikana na mtungi uliokuwa na mafuta ya petroli.

Share news tips with us here at Hivisasa

Inadaiwa kuwa watatu hao walikuwa na nia ya kuteketeza chumba cha maakuli shuleni humo.

Akithibitisha kisa hicho siku ya Ijumaa, naibu mkuu wa polisi eneo la Kisauni Bw Walter Abondo alisema kuwa wanafunzi hao walipatikana na lita moja ya petroli.

Watatu hao wanazuiliwa katika Kituo cha polisi cha Bamburi, huku polisi wakiendela na uchunguzi kwa kina.

Mikasa ya moto katika shule za upili yanaendelea kuwanyima usingizi wadau katika sekta ya elimu nchini huku muungano wa walimu wa Kuppet ukitaka shule zote kufungwa ili kuzuia mikasa zaidi.

Aidha, Kuppet imetishia kugoma kupinga kukamatwa kwa baadhi ya walimu kwa kuhusishwa na visa hivyo vya moto.

Wakuu wa usalama wameonya wauzaji wa mafuta aina ya petrol dhidi ya kuwauzia watu wasiokuwa na vitambulisho mafuta hayo.