Mbunge wa Subukia Nelson Gaichuhie amewarai wanahabari kutoka kaunti ya Nakuru kutumia nyadhifa zao kuelimisha vijana kuhusu umuhimu wa amani.
Akizungumza na wanahabari ofisini mwake siku ya Jumatatu, Gaichuhie alisisitiza umuhimu wa amani kwani amani uleta wiyano katika taifa.
"Tunapowakilisha siku ya amani duniani, ningependa wanahabari wawajuze vijana umuhimu wa kuishi na umoja na amani, ili nchi iweze kusonga mbele,” alisema Gaichuhie.
Septemba 21 ni siku inayosherekewa kila mwaka kote duniani ili kukumbuka walio saidia kuleta amani katika nchi tofauti tofauti.
Kulingana na mbunge huyo, siku ya amani yafaa kusherehekewa na vijana katika shughuli za kiraia, na kuimarisha amani na utulivu katika nchi.
Bwana Gaichuhie alisema kuwa mafunzo kuhusu amani yatasaidia vijana kujielewa na kuwa mstari wa mbele katika kutetea taifa lao.
Serikali ya jimbo la Nakuru, imeandaa msafara wa kuzuru maeneo tofauti tofauti katika kaunti ya Nakuru ambapo vijana watahusishwa kwa kufunzwa jitihada zao katika jamii.
Kulingana na waandalizi wa tamasha hilo, kati ya vijana watakao funzwa ni pamoja na wale walioyapa maswala ya amani na kutetea haki za binadamu kipau mbele.