Vyombo vya habari vimepewa changamoto kuangazia mno swala la unyanyapaa dhidi ya wanawake ili kutokomeza swala hilo katika jamii. Wito huo ulitolewa na afisa wa polisi Washingtone Akala anayesimamia kitengo maalumu cha afya kuhusu Ukimwi katika kituo cha polisi cha Kasarani Nakuru.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Katika mahojiano Jumatano, Akala alisema kuwa kuna visa vingi vya unyanyapaa na dhuluma dhidi ya wanawake humu nchini lakini havijaangaziwa.

"Nyinyi wanahabari mna wajibu mkuu katika jamii, mnafaa kuanika maovu haya na mfuatilie kikamilifu ili haki ipatikane,"alisema.

Wakati huo huo, Akala alishtumu vikali baadhi ya jamii ambazo zingali zinakumbatia tamaduni potovu zilizopitwa na wakati.

Aliongeza kuwa jamii,wanahabari na viongozi wa kidini wanafaa kushirikiana katika kumaliza maovu hayo.

Ni matamshi yaliyoungwa mkono na afisa wa polisi Halima Ore anayejihusisha na afya ya wanawake katika kituo cha polisi cha kasarani Nakuru.

Alisema kuwa la muhimu ni jamii kuja pamoja na kuzungumza lugha moja ya kuangamiza unyanyapaa.