Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama amewataka wanakandarasi waliopokezwa kandarasi za kujenga soko tano katika kaunti ya Nyamira kumaliza ujenzi huo kwa haraka. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Akihutubu wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa soko la Ikonge siku ya jumatatu, Nyagarama alisema kuwa yafaa wanakandarasi waliolpokezwa kazi ya ujenzi wa soko kumaliza ujenzu huo kwa haraka  ili wafanyabiashara waweze kuendesha shughulu zao bila matatizo. 

"Wafanyabiashara wana hamu ya kumalizika ujenzi wa soko huku Nyamira ili iwawie rahisi kuendesha shughuli zao za kila siku, na hilo halitowezekana iwapo wanakandarasi hawatokamilisha ujenzi huo kwa wakati," alisema Nyagarama.

Akizungumzia suala la kina mama wafanyabiashara rejareja kujistawisha, Gavana Nyagarama aliwasihi kina mama kujiunga kwenye makundi ya kupokezana mikopo. 

"Kina mama ni watu mhimu sana kwa ukuaji wa taifa hili, na ningependa kuwahimiza wajiunge na vikundi vya kupokezana mikopo ili kujiendelesha kwa maana hakika nikupitia kwa vikundi jamii inaweza kujistawisha," alisema Nyagarama.