Muungano wa wanakandarasi katika kaunti ya Kisii wametishia kuandamana juma lijalo iwapo serikali ya kaunti hiyo haitawalipa pesa zao walizofanyia kazi mwaka 2013/2014, 2015/ 2016.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakihutubia wanahabari mnamo siku ya Alhamisi mjini Kisii, mwenyekiti wa muungano huo wa wanakandarasi katika kaunti ya Kisii Kennedy Mariera walisema serikali hiyo haijawalipa pesa zao, na kusema juma lijalo wataandamana hadiafisi za gavana wa kaunti hiyo James Ongwae kulazimisha kulipwa pesa zao.

Kulingana na Mariera, muungano huo unamiliki wanachama 200 halisi,  huku akisema wengi wanaishi katika maisha duni kufuatia kutolipwa pesa zao .

“Pesa ambazo tulifanyia kazi kwanzia mwaka 2013 hadi sasa tunaomba tulipwe kile tunahitaji kutoka kwa gavana ni pesa zetu,” alisema Mariera.

Wakati huo huo, Mariera alisema kuna baadhi ya watu ambao hudai kuwa wanakandarasi katika kaunti hiyo ambao huegemea upande wa gavana, huku onyo kali ikitolewa kwao kwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwani hawana cheti cha kuonyesha kuwa wao ni wanakandarasi halisi wa kaunti hiyo ya Kisii.