Kamishena wa kaunti ya Kisii chege Mwangi amewaomba wakaazi walioshika vitambulisho katika ofisi ya huduma Center iliyoko mjini Kisii kuchukua vitambulisho vyao.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza siku ya Jumatatu kwa hafla ya kusherehekea siku kuu ya madaraka katika uwanja wa gusii stadium Kamishena Mwangi alisema vitambulisho viko katika huduma center ilioko mjini Kisii ni vingi kupita kiasi na kusema vitambulisho hivyo ni zaidi ya 450.

“Huduma center ilikuja isaidie watu maana ukishika kitambulisho kinatayalishwa haraka mbona mnashika vitambulisho na hamvichukui?” auliza Chege.

“Nawaomba wale walishika vitambulisho muende mchukue kutoka kwa huduma center maana ni wengi wanaendelea  kuvishika vitambulisho hivyo,” aliongezea Mwangi.

Wakati uo huo, kamishena huyo aliwaomba wakaazi wa kaunti ya Kisii kukumbatia mradi wa nyumba kumi ili kuweka usalama wa kutosha kwa wananchi wa Kenya.

“Usalama huanza na wewe ndio maana nawaomba kila mwananchi kuupea mtadi wa nyumba kumi kipao mbele ili uhalifu usishuhudiwe katika eneo la Kisii,alidokeza Kamishena Mwangi.

Aidha, alisema kila mtu sharti amjue wanayeishi naye awe jilani awe rafiki na kusema hiyo itakuwa njia mojawapo ya kupunguza visa vya uhalifu nchini.