Wakaazi  wa Matunwa wadi ya Gesima kaunti ya Nyamira wamempongeza mwakilishi  wa wadi  hiyo Kennedy Nyameino kwa ujenzi wa barabara ya Gesima-Bokione ambayo imekuwa ya manufaa kwao.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Salome Kenyoni mwanabiashara katika soko lo Gesima amesema kuwa ni vizuri wanasiasa kuwa wanatimiza ahadi walizozifanya wakati wa kampeini.

“Nataka kumshukuru mbunge wetu kwa sababu ametimiza mengi ya yale aliyotuahidi wakati wa kampeini,” asema Kenyoni.

Kwa sasa Kenyoni amemwomba mbunge huyo kutengeneza barabara mingi katika sehemu hiyo ili kuinua viwango vya uchukuzi.

Kwingineko wazazi wa shule ya msingi ya Matutu wamempongeza mbunge wa Kitutu Masaba, Timothy Bosire, kwa kusaidia katika ujenzi wa shule hiyo.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Patrick Nyangeri, amesema ujenzii wa madarasa mapya unaendelea na hivi karibuni utakuwa umemalizika.

Nyangeri pia aliwaomba wazazi kushirikiana katika ujenzi huo ili watoto wao wapate mahali pazuri pa kusomea.

Mjengo huo unaendelezwa na hazina ya maendeleo ya maeneo bunge (CDF) ya eneo bunge hilo.