Wananchi wamehimizwa kuwa macho dhidi ya vyama ambavyo hutoa mikopo kwao ili kuzuia kulaghahiwa.
Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa baadhi ya vyama hutoa mikopo kwa wananchi katika kisha baadaye huja nyakati za usiku kama wezi na kuwanyanganya pesa hizo.
Akizungumza siku ya Jumatatu mjini Kisii mwenyekiti wa chama cha Wakenya Pamoja Sacco, Grace Omare alisema visa vya aina hiyo vimekuwa vikiripotiwa kwa muda mrefu sasa.
Kulingana naye wananchi wanastahili kupata mafunzo dhidi ya mikopo hiyo kabla ya kukabidhiwa na vyama ambavyo havijulikani.
Pia aliomba wananchi kukopa kutoka vyama ambavyo vimejisajili katika benki mbalimbali kuzuia ulaghai huo ambao hutekelezwa na watu wakorofi.
“Wananchi wengi wamekuwa wakipata hasara kubwa maana imejulikana kuwa kuna baadhi ya vyama ambavyo hutoa pesa kwa wananchi," alisema Omare.
"Kisha wanachama hao wanakuja nyakati za usiku kwa yule aliyepewa mkopo na kumnyanganya baadaye wanadai pesa hizo,” aliongeza Omare.
“Yeyote anahitaji mkopo sharti afuatilie ikiwa chama hicho kinachohitaji kutoa mkopo kimesajilikwa kwa benki au la,” aliongeza Omare.