Wito umetolewa Kwa wakaazi wa wadi ya Kivumbini Nakuru mjini mashariki kujitokeza na kutoa mchango wao kuhusiana na makadirio ya bajeti mwaka huu wa kifedha. Akizungumza wakati wa kikao cha wananchi kutoa maoni kuhusu bajeti katika ukumbi wa kijamii Kivumbini, afisa msimamizi wa wadi hiyo Gitonga Kinyanjui alisema kuwa vikao hivyo ni muhimu kwani wananchi hupata fursa ya kutoa mchango wao.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Aliongeza kuwa kwa mujibu wa katiba, wananchi wanafaa kupendekeza miradi yao kabla ya kutengewa fedha kufanikisha.

"Ombi langu ni moja kwamba wananchi waendelee kujitokeza katika vikao vya mchakato wa bajeti ili maslahi yao yaweze kuzingatiwa,"alisema Gitonga.

Wakati huo huo aliwahakikishia wakaazi kwamba serikali iko tayari kupiga jeki miradi yote itakayopendekezwa na mwananchi.

Mkutano huo ulileta pamoja mitaa mbalimbali ya wadi hiyo.