Watu wanaoishi na virusi vya ukimwi katika kaunti ya Kisii na ile ya Nyamira wamezipa serikali zao changamoto kuhusu umuhimu wa kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa huo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Waadhiliwa wengi bado wanasema kuwa kuna hatua ambazo zafaa kuchukuliwa kwenye vita dhidi ya maradhi hatari ya ukimwi.

Wengi walio na virusi vya HIV katika maeneo hayo wanasema kuwa jamii zao huwabagua punde tu wanapotabua hali zao.

Kwa sasa wakaazi hao wanahisi kuwa serikali pamoja na vikundi visivyo vya kiserikali vyapaswa vitie bidii katika vita dhidi ya ukimwi.

Josephine kwamboka* ni mama mjane ambaye ameishi na virusi hivyo kwa zaidi ya kipindi cha mwongo mmoja na nusu na anasema kuwa kutokuwepo na mashirika yaliyojitolea kupambana na janga hili ndio tatizo kuu inakumba vita hivi.

Kwamboka anadai kuwa pindi alipoanza kuwa wazi kuhusu hali yake amekuwa akipokea waadhiliwa wengi, kwa njia ya siri, ambao wanataka ushauri wake.

"Waadhiliwa wengi huogopa kubaguliwa baada ya hali zao kujulikana. Ni vyema kwa jamii kukubali uwepo wa janga hili na kuwa wazi na wenzao hasa wanapogundua kuhusu hali za jamaa zao,” asema kwamboka.

Kwamboka anawasihi walio na watu ambao wanadhiliwa na virusi hivi kusimama na wao kwa hali na mali.

"Wakati mwingine ukigudua kuwa dada, ndugu au mzazi wako ameambukizwa virusi hivi unapaswa umsaidie uwezavyo,” asema Kwamboka.

Kwamboka pia anawasihi wanao kaa karibu na wenye virusi vya ukimwi kuwa shauri ili wajikubli.

Kwa sasa Kwamboka ako na kikundi ambacho kinawatembelea watu wanaoishi na virusi vya ukimwi na kuwahimiza.

“Changamoto kubwa eneo hili ni kuamini uchawi, taasubi za kiume ambazo wanaume wanaamini kwamba ugonjwa huo huletwa na kina mama, utawala wa mkoa kutounga mkono juhudi za kupambana na maradhi haya na woga wa kujieleza,” alisema Kwamboka.

Alitoa shukrani zake kwa shirika la internews kwa kumpiga jeki katika harakati zake za kupambana na ukimwi kwa njia ya upashaji habari katika mpango wake wa awamu ya kwanza.

Kwamboka anasema kuwa kwa sasa katika eneo analotoka la Omogonchoro watu wameanza kuwa wazi kuhusu hali zao.

 Kwa sasa Kwamboka ameipa serikali changamoto kupitia kwa wizara ya afya kujitolea kuweka mikakati maalum ambayo itasaidia kupunguza kuenezwa kwa virusi vya ukimwi.