Share news tips with us here at Hivisasa

Mshirikishi mkuu wa Usalama katika Ukanda wa Pwani, Nelson Marwa, amewalaumu wanaofanya biashara ya kununua magari kutoka nje ya nchi kwa kuingiza dawa za kulevya nchini..

Akizungumza na wanahabari katika afisi yake siku ya Alhamisi, Marwa alisema wafanyibiashara hao hutumia sehemu za magari kuficha dawa kama vile heroine na cocaine ili siziweze kujulikana na maafisa wa usalama katika Bandari ya Mombasa.

Aidha, Marwa alisema kuwa tayari serikali imepata habari hizo na iko imara kukabiliana na janga hilo, kwani limezidi kusheheni katika sehemu ya Pwani.

Aidha, Marwa amewataka makamishna wa kaunti kuchukua hatua za haraka, kwa kuwa eneo la Pwani huenda likapoteza watu watakaohitajika baadae katika taifa hili.