Wakaaji wa mji wa Kisii na viunga vyake kaunti ya Kisii wameombwa kudhumisha usafi ili kujikinga kutokana na magonjwa mbalimbali.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea wakati alipokua akiwapongeza  wanaofanya usafi katika mji wa kisii,  maeneo ya mwembe mhudumu wa afya ya jamii [community clinical officer] ambaye tena ni mwenyekiti wa wahudumu hao King’oina Kepha amesema viwango vya usafi vimeongezeka kwa asilimia 85%.

Kepha amesema tangu chama cha Muungano Minto Youth  waaze kusafisha mji wa Kisii na viunga vyake kumekuwa na mabadiliko makubwa na sasa mji huo una sura mpya,  kitu kinachowafuraisha wakaazi wengi na biashara sasa zinafanywa kwa njia swali.

Amewaomba wakaaji kushirikiana na wahudumu hao hili kuinua viwango hivyo zaidi,huku akiwakashifu baadhi ya watu ambao hutupa uchafu kiholelahole kwa kile wanachosema hata wakitupa pahali popote kuna watakaotoa.Wengi wa watu hao ni wale wanao magari yao ya  binafsi ambao hutupa uchafu huo ili kuepa kulipia uchafu huo  kuchukuliwa pahali panasthaili na wahudumu hao.

“Kuna watu wengine ambao uchukua uchafu wakati wa usiku na kutupa pahali ambao hapasthaili hii nikutokana nakutotaka kulipa manispaa ya Kisii  [county council] ili  kuchukua uchafu wao kutoka pahali wanamoishi na wengi wao kutumia magari yao,”alieleza Kepha

Siku za wanaofanya kitendo hicho zinahesabiwa huku watakaposhikwa watachukuliwa hatua za kisheria.

Kwingineko wahudumu hao wanaofanya usafi wamelalama kutokana na changamoto  wanazokumbana nazo kutoka na mifereji ya kupeleka uchafu[sewage].Imelipotiwa mara kwa mara mifereji hiyo upazuka na kushababisha harufu mbaya  na kuwapelekea kupata  kazi ngumu wanapofanya usafi wao.Kulingana na wao sehemu  nyingi mifereji upazuka  kama maeneo ya njia ya kuelekea Cathedal,kando ya barabara ya jengo la Elimu complex,barabara ya kuelekea chuo kikuu cha kisii .

Aidha, wamewaomba wanaoweka mapomba ya uchafu kutoyaelekeza kwa njia ambayo inaweza kusababisha madhara kwa wananchi.