Wakaaji wa mji wa Kisii na viunga vyake kaunti ya Kisii wameombwa kudhumisha usafi ili kujikinga kutokana na magonjwa mbalimbali.
Akiongea wakati alipokua akiwapongeza wanaofanya usafi katika mji wa kisii, maeneo ya mwembe mhudumu wa afya ya jamii [community clinical officer] ambaye tena ni mwenyekiti wa wahudumu hao King’oina Kepha amesema viwango vya usafi vimeongezeka kwa asilimia 85%.
Kepha amesema tangu chama cha Muungano Minto Youth waaze kusafisha mji wa Kisii na viunga vyake kumekuwa na mabadiliko makubwa na sasa mji huo una sura mpya, kitu kinachowafuraisha wakaazi wengi na biashara sasa zinafanywa kwa njia swali.
Amewaomba wakaaji kushirikiana na wahudumu hao hili kuinua viwango hivyo zaidi,huku akiwakashifu baadhi ya watu ambao hutupa uchafu kiholelahole kwa kile wanachosema hata wakitupa pahali popote kuna watakaotoa.Wengi wa watu hao ni wale wanao magari yao ya binafsi ambao hutupa uchafu huo ili kuepa kulipia uchafu huo kuchukuliwa pahali panasthaili na wahudumu hao.
“Kuna watu wengine ambao uchukua uchafu wakati wa usiku na kutupa pahali ambao hapasthaili hii nikutokana nakutotaka kulipa manispaa ya Kisii [county council] ili kuchukua uchafu wao kutoka pahali wanamoishi na wengi wao kutumia magari yao,”alieleza Kepha
Siku za wanaofanya kitendo hicho zinahesabiwa huku watakaposhikwa watachukuliwa hatua za kisheria.
Kwingineko wahudumu hao wanaofanya usafi wamelalama kutokana na changamoto wanazokumbana nazo kutoka na mifereji ya kupeleka uchafu[sewage].Imelipotiwa mara kwa mara mifereji hiyo upazuka na kushababisha harufu mbaya na kuwapelekea kupata kazi ngumu wanapofanya usafi wao.Kulingana na wao sehemu nyingi mifereji upazuka kama maeneo ya njia ya kuelekea Cathedal,kando ya barabara ya jengo la Elimu complex,barabara ya kuelekea chuo kikuu cha kisii .
Aidha, wamewaomba wanaoweka mapomba ya uchafu kutoyaelekeza kwa njia ambayo inaweza kusababisha madhara kwa wananchi.