Reli ya kisasa ya SGR. [Photo/ mediamaxnetwork.co.ke]
Washukiwa 11 wanaodaiwa kuiba vyuma vya reli ya kisasa ya SGR wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni sita ama shilingi milioni tatu pesa taslimu kila mmoja.
Washukiwa hao ni Peterson Senteu Matunda,Theophilas Mwongela Kilivu, Bernard Maina Rukungu, Joseph Mbugua, James Ndichu Mburu, Wilbrod Omondi, Joel Kabiru, Mugi Nyaga, Moses Wanyama Namulanda, David Musyoki Nzili na Nicholas Muthuka John.Mahakama ilielezwa siku ya Jumatatu kuwa washukiwa hao wanadaiwa kutekeleza kisa hicho mnamo May 26, 2017 katika eneo la Kavinduni huko Mwavumbo, gatuzi dogo la Kinango.Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Lilian Lewa.Kesi hiyo itatajwa tena Juni 19 mwaka huu.