Wakazi wa mtaa wa Nyanchwa mjini Kisii wamewaomba wanaopewa kandarasi ya kujenga nyumba katika eneo hilo kutoweka mchanga barabarani wakisema mchanga huo huziba barabara na kusababisha msomgomano wa magari.
Wakiongea siku ya Jumamosi na Mwaadishi huyu katika mataa wa Nyanchwa, Wadi ya Kisii ya Kati, eneo bunge la Nyaribari Chache katika Kaunti ya Kisii, wakazi hao walishtumu kandarasi hao kwa kuweka mchanga na udongo huo wanaochimba kutoka mahali waokojenga na kuuweka katika barabara zilizoko karibu.
Wakazi hao walisema udongo huo umekuwa ukiwasumbua haswa wakati wa mvua kwa kuwa mvua usomba udongo huo na kuchafua maji katika mito zilioko karibu na eneo hilo na maji hayo ndio watu hutumia katika shughuri zao za kila siku.
“Naomba wanaofanya kazi ya ujenzi katika eneo hili kutoweka udongo katika barabara kwani tunasumbuka wakati tunapita,” alisema Edward Kiage, mkazi.
Aidha, waliwaomba wamiliki wa nyumba hizo zinaojengwa katika eneo hilo kuwaelezea kandarasi hao mahali udongo huo unastaili kuweka ili kuutoa katika barabara hilo ili kurahisisha uchukuzi katika eneo hilo.