Mbunge wa eneo Bunge la Kitutu Masaba, Kaunti ya Nyamira Timothy Bosire amewaomba Askari wa utawala na Machifu kufanya uchungunzi kuhusu wale wana tabia ya kulima na kupanda mgomba wa ndizi kwenye barabara za eneo bunge hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea siku ya Jumamosi katika shule ya upili ya Rigomba iliyoko eneo bunge lake iliyochomeka mwenzi moja uliopita na kuifadhili Sh900,000 ili kujenga bweni mpya, Mbunge Bosire aliwaomba Askari pamoja na machifu kuwakamata na kuchukuliwa hatua za Kisheria wanaochimba barabara wakidai ni njia moja ya kulalamikia barabara mbovu.

“Yeyote atakayepatikana na kosa la kuharibu barabara za umma katika eneo bunge langu kwa kulima atiwe mbaroni na achukuliwe hatua kali za kisheria,” alisema Bosire.

Wakati uo huo,  Mbunge huyo aliwakosoa vikali wale wanafanya uharibifu huo wa barabara na kusema ni kukiuka sheria za nchi ya Kenya.

“Kuna habari nilipokezwa kuwa pia kuna baadhi ya viongonzi huona uharibifu huo ukifanywa na hawachukui hatua yoyote na kusema hawajali. Nataka niwambie kuwa kama kiongozi, haifai kuona wananchi wakifanya makosa na ukose kuwaonya dhidi ya kitendo hicho ambacho kinakiuka sheria,” alidokeza Mbunge Bosire.