Share news tips with us here at Hivisasa

Tume ya kitaifa ya NLC ardhi imekutana na wamiliki wa ardhi zilizo kwenye eneo ambapo ujenzi wa reli mpya ya kisasa unaendelea.

Akizungumza na wanahabari wakati wa mkutano na wamiliki hao mjini Mombasa siku ya Jumanne, mwakilishi wa tume hiyo Abigael Mbagaya alisema watu wengi wamekuwa wakisusia mikutano yao jambo linalolemaza shughuli hiyo.

“Huu ndio mkutano wetu wa mwisho tunafanya lakini tatizo watu wakiitwa hawataki kuja, inakuwa vigumu kwetu hata kuendesha shughuli ya kuwafidia na ikizidi tutaregesha pesa kwa serikali.” Alisema Bi.Mbagaya.

Pia vile vile afisa huyo aliwaonya watu dhidi ya kununua ardhi zilizo karibu na ujenzi wa reli kabla ya kushauriwa na tume hiyo ya ardhi.