Takribani wanaoendesha Bodaboda 300 kutoka Kaunti ya Kisii wanatarajiwa kupata mafundisho katika mwaka huu kuhusu uhusiano bora kati yao na wateja.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza na mwandishi huyu wa Habari siku ya Jumanne, Mwenyekiti wa wenye Bodaboda hao Michael Mose alisema kuwa mafundisho hayo yatakuwa ya muhimu ili kuwasaidia wanaoendesha Bodaboda kuwa na maadili mema katika utendakazi wao.

Mose ameiomba Kaunti ya Kisii kuwasaidia katika maandalizi ya mafundisho hayo ambayo alisema yanatarajiwa mwishoni mwa mwaka huu.

“Tunatarajia kuandaa mafundisho kwa wanaoendesha Bodaboda 300 mwaka huu kutoka 200 ambao walipata mafundisho mwaka jana,” alisema Mwenyekiti Mose.

Mose alisema kuwa mradi hiyo inakusudia kupunguza visa vya utovu wa nidhamu miongoni mwa wenye Bodaboda hao.

Tunaiomba Kaunti ya Kisii kupitia kwa Gavana wetu James Ongwae kutusaidia katika maandalizi ya mafundisho hayo maanake inakuwa ni ya gharama kubwa na sisi wenyewe hatutaweza kuyagharamia,” alirai Mose.

Aidha, aliipongeza Serikali ya Kaunti kwa kutoongeza ada inyotozwa wanaoendesha Bodaboda na pia kuiomba kuwasaidia wanachama wa Bodaboda kifedha ili waweze kuanzisha miradi mbalimbali ya kujikimu kimaisha.