Serikali ya kaunti ya Mombasa imeahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria wanaounganisha maji kwa njia ya magendo na kuwauzia wakazi pamoja na kukwepa kulipa ushuru kuwa watakabiliwa kisheria kwani kuharibu uwekezaji wa kaunti hiyo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kaimu waziri wa Mazingira, Maji na Raslimali katika kaunti ya Mombasa Tendai Lewa amesema kuwa tayari serikali ya kaunti imepata habari kuhusu mawakala wanaowaunganishia wakazi maji kwa njia ya mkato ili kukwepa kulipa ushuru na lazima hatua hiyo kusitishwa.

Amesema kuwa tayari maafisa wa serikali ya kaunti hiyo wametumwa nyanjani kuchunguza wanatekeleza wizi huo wa maji ili kuchukuliwa hatua na kuahidi hata kuwafikisha mahakamani kwa kuhujumu mali ya umma na kukwepa kulipa ushuru.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumatatu, Tendai alisema kuwa zaidi ya asilimia 30 ya ushuru wa kaunti unaingia kwa mifuko ya baadhi ya mawakala wanaofuja mali ya umma na akasema kuwa juhuzi hizo zinakomeshwa.

“Tumegundua baadhi ya wakazi wanaunganisha maji kwa njia ya mkata na kusababisha uhaba wa maji Mombasa na katika kaunti yetu kwa jumla, na tunawachukuza kwani sheria lazima ichukua mkondo wake na kuwafungulia mashtaka mahakamani,” alisema Tendai.

Hata hivyo, aliahidi kukabiliana na uhaba wa maji katika kaunti hiyo ya Mombasa na kuhakikisha kuwa changamoto wanazopitia wakazi kufuatia uhaba wa maji zinakabiliwa.

Picha: Kaimu Waziri wa Mazingira, Maji na Raslimali kaunti ya Mombasa Tendai Lewa akitoa onyo kwa wanaounganisha maji kwa njia ya magendo kuwa watakabiliwa kisheria.