Wafanyibiashara wanaouza bidhaa gushi katika kaunti ya Kisii wameonywa dhidi ya kuuza bidhaa hizo na kuombwa kufanya biashara kwa njia halali.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea  hiyo jana katika uga wa Gusii katika hafla ya kusherekea siku kuu ya Madaraka, mwenyekiti wa wafanyibiashara Benjamin Onkoba aliwaonya wanabiashara  wote wanaouza bidhaa hizo.

“Kuna wanabiashara wengine katika kaunti hii yetu ambao wanauza bidhaa gushi na wanatumia njia ya mkato ambayo hakubaliki, ninawaomba watu kama hao wabadilishe tabia hiyo,” alihoji mwenyekiti Onkoba.

Kwingineko, aliwaomba wanabiashara wote kutumia njia mbadala ya kutoa malalamishi yao kwa wasimamizi wao ili shida zao kutatuliwa, na kuwaomba kuwa kuenda katika maandamano si njia ya kuleta uhusiano mwema.

“Wakati shida zimetokea tunaomba kuwa muwe mnawasilisha malalamishi yenu kwetu ili suluhu ya haraka na mapema kutafutwa ili kupata jibu, lakini kuenda katika  maandamano si suluhu na hiyo ni njia ya kurudisha maendeleo nyuma,” aliongezea Onkoba.

Aidha, alipongeza serikali ya kaunti kwa kuweka mataa katika mji wa Kisii na viunga vyake, huku akisema wanabiashara wamefaidika pakubwa.

Aidha, aliwaomba wawekezaji Zaidi kuwekeza katika mji huo, huku akisema kuna mazingira mema ya biashara.