Siku moja baada ya taarifa kuenea katika vyombo vya habari nchini Alhamisi hii kuhusu kuondolewa kwa walinzi wa gavana wa Mombasa Hassan Joho, mwanasiasa mwingine kutoka eneo hilo amejitokeza na kusema kuwa pia nae amepokonywa walinzi.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nasir mapema Ijumaa aliandaa mkutano na wananchi kueleza kile kilichomkuta asubuhi ya kuamkia siku hiyo.

Huku akiongea kwa masikitiko, Nasir alidai kuwa aliamka na mshtuko baada ya kugundua kwamba mlinzi wake wa kipekee ameondolewa bila kupewa taarifa yoyote.

Aidha mbunge huyo amesisitiza kuwa masaibu wanayopitia yeye pamoja gavana wa Mombasa ni njama ya serikali baada ya chama cha ODM kushinda katika uchaguzi mdogo wa Malindi mapeka wiki hii.

“Hii ni njama tu ya kunikandamiza baada ya ule uvhaguzi wa Malindi lakini hakuna jambo litakalotuzuia kuongea ukweli,” alisema Nassir.

Wakati huo huo mbunge huyo watafanya kila niia kuhakikisha kwamba wanapigana na ufisadi unaoendelea katika serikali.

Masaibu ya Nassir yanakuja huku naye Joho akiendelea kulaumu serikali baada ya polisi kuwaondoa walinzi wake siku ya Alhamisi huku ikidaiwa kwamba walienda kwa masomo zaidi.

Hata hivyo hatua hiyo imehusishwa na siasa ambapo kwa muda sasa kumekuwa na uhasama mkubwa baina ya serikali na upande wa upinzani juu ya ubabe wao wa kisiasa katika ukanda wa Pwani.